Thursday, 17 July 2008

RONALDO"HERE SOON"

Rais wa club ya Real Madrid Ramon Calderon amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa Ronaldo yupo njiani kutua katika klabu hiyo hivi karibuni.Raisi huyo wa Madrid aliyasema hayo bila kutoa maelezo zaidi juu ya lini winga huyo anaweza kutua rasmi Madrid.

kwaheri Arsenal f.c!!!!!!!!!!

kiungo alieichezea arsenal kwa mda usiopungua miaka 6 Gilberto Silva amekamilisha uhamisho wake kwena panathenaiko ya ugiriki kwa kitita cha paundi milioni 8.huyu ni mchezaji wa 3 kuondoka baada ya jana kiungo kutoka Belarous A.Hleb kutimkia F.C.Bercelona.

Friday, 30 May 2008

Enzi za urafiki wa bush na saddam


kadri watu wanavvyozidi kuwa pamoja ndivyo wanavyozidi kuzoeana,Bush na al marhum Saddam Hussein walikua marafiki wakupigiwa mfano,kama ilivyo siku hazigandi,Bush akamchenjia Saddam kwa kumfungulia kesi isiyo na ushahidi na kulazimisha Saddam auwawe bila hatia huku akidai anamiliki silaha za hatari nchini Iraq.

Monday, 7 April 2008

sio inshu maselaaa!

SSio inshu hata kidogo eti unampotezea kiumbe mwezako uhai wake eti kwasababu ya nyama!Kama nyama zipo nyingi tena tamu kuliko za binaadamu,iiweje unazikacha zote hizo na kung'ng'nia kupoteza maisha ya vichanga visivyo na hatia yoyote ile?Inasikitisha kupita maelezo si tu kwa kuona bali hata kusikia upuuzi huo kwani ni kinyume na haki za kabinadamu.Tubadilike jamani

prf Jay angatuka!

Msanii wa miondoko ya kizazi kipya Proffesa Jay juzi alizindua Album yake mpya katika ukumbi wa Dimond Jubelee akisindikizwa na wasanii wenzake kibao wakiwemo A.Y,Mwana FA pamoja na wengine wengi.prf Jay anatamba na wimbo wake mpya ujulikanao kama "Nan'gatuka".

MUONEKANO WA NDANI WA KAABA


Picha ikionesha muonekano wa ndani wa kijumba kitakatifu(al kaaba)kilichopo katika nchi ya Saud Arabia.Waislamu wenye uwezo wanakwenda kuhij Makka kila baada ya mwaka mmoja.